Posts

Showing posts from August 20, 2023

KAMATI YA LAAC YARIDHISHWA MRADI WA KITEGA UCHUMI WA BIL. 18 JIJI LA DODOMA

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeridhishwa na ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi Mtumba kwa shilingi bilioni 18 lililojengwa kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani ya Halmshauri ya Jiji la Dodoma. Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Stanslaus Mabula Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Stanslaus Mabula baada ya kupokea taarifa ya Jengo la Kitega Uchumi Mtumba la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa kisasa wa mikutano wa halmashauri hiyo. Mabula alisema “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, tumesikiliza taarifa zote tatu. Kwanza niwapongeze sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufikiria kuwa na vitega uchumi ambavyo kiukweli vitaipaisha halimashauri hii. Sisi kama Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, tumekuwa na msisitizo kila wakati kwanza kuhakikisha halmashauri nchini zinaongeza mapato yake. Pili, zibuni vyanzo vingi zaidi ili ziweze kuon...