DC Shekimweri ataka wananchi washirikishwe katika ujenzi wa Mji wa Kisasa Hombolo

Na. Coletha Charles, DODOMA

Wananchi, sekta binafsi na makundi mbalimbali wametakiwa kushirikishwa katika maandalizi ya Mji wa Kisasa wa Hombolo (HOTSAC), ili wanufaike na fursa za kiuchumi zitakazotokana na mradi huo.



Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabiri Shekimweri, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa upembuzi yakinifu na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Hombolo, Chinangali Park, jijini Dodoma.

Alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kufungua fursa za ajira, biashara, ujenzi, viwanda na huduma, hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa mapema kuzitumia fursa hizo wakati wa utekelezaji na baada ya kukamilika.

Alisisitiza kuwa umuhimu wa kuandaa mpango wa usimamizi wa wadau na kushirikisha wataalamu wa ardhi ili kudhibiti matumizi yasiyopangwa, kuzuia migogoro na kuhakikisha maendeleo yanazingatia Mpango Kabambe wa Hombolo.

 


Kwa upande wake, Mkazi wa Kata ya Hombolo Makulu, Jiji la Dodoma Agness Matiko alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kuleta maendeleo kwa wakazi wa eneo hilo, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha katika hatua za maandalizi yake.

Aliongeza kuwa wananchi wanatarajia kupata elimu kuhusu fursa zitakazotokana na mradi huo, hususan ajira, biashara na uwekezaji, ili waweze kujiandaa mapema na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Hombolo.

Mafanikio ya mradi huo yatategemea ushirikiano wa viongozi, wataalamu na wananchi, akihimiza kila mdau kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha Hombolo inakuwa kitovu kipya cha maendeleo, uwekezaji na ukuaji wa uchumi jijini Dodoma.




Comments

Popular Posts

KATA YA CHAMWINO YATEKELEZA AGIZO LA USAFI WA MAZINGIRA

Agenda ya Lishe yaongeza Ari ya usomaji S/M Dodoma Makulu

KATA YA CHAMWINO YATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA