Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ahimiza matumizi ya mfumo NeST
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko aeleza kuwa mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma NeST katika kufanya manunuzi ya vifaa vya serikali ni mfumo rafiki unaorahisisha manunuzi na kuweka taarifa hizo katika hali ya usalama. Aliyazungumza hayo katika Baraza la Madiwani la kawaida liliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa madiwani. Alisema kuwa mfumo wa manunuzi wa NeST upo tayari kwa mujibu wa sheria na umeonyesha matokeo chanya. “Niwajulishe ndugu wajumbe ya kwamba, mfumo huu hatuna namna ya kuepuka kuutumia kwasababu ndio mfumo ambao tunapaswa kuwa nao ili kufanikisha manunuzi ya vifaa mbalimbali vya serikali” alisema Dkt. Sagamiko. Aliongeza kuwa mfumo haumlazimishi mnunuzi kununua kila kitu kwa wakati mmoja. “Mfumo huu unahitaji ushirikiano ili uweze kufanya manunuzi yako. Kikubwa ni wewe kuhakikisha unafahamu unafanya manunuzi ya kiwango gani. Hakikisha unafahamu...