KATA YA CHAMWINO YAADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI

Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO KATA ya Chamwino yaadhimisha maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo. Akiongelea maadhimisho hayo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa kufanya usafi wa mazingira katika barabara inayotoka makutano ya Wajenzi mpaka kona ya Viva la vida. Alisema kuwa usafi huo ulihusisha kusafisha mtaro wenye urefu wa mita 1,500. “U safi wa mazingira pia ulifanyika katika mitaro yote inayozunguka Shule ya Sekondari ya Hijra na wananchi walijitokeza na kufanya usafi katika korongo karibu na uwanja wa Shell Complex. Zaidi ya kusafisha mitaro, usafi huo ulihusisha kutoa taka ngumu na kuokota makopo na mifuko kwenye mtaro na maeneo ya pembezoni mwa barabara na korongo” alisema Nkelege . Akiongelea mafanikio ya maadhimisho Siku ya Usafi Duniani, alisema kuwa yametokana na ushirikiano wa karibu na wadau mbalimbali. “Napenda kutoa shukurani ...