Posts

Showing posts from June 17, 2025

Halmashauri ya Jiji la Dodoma yashiriki maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma inashiriki maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayojumuisha Taasisi za Serikali, Bunge na Mahakama, katika uwanja wa Chinangali Park jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yanalenga kuonesha uwajibikaji wa taasisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kutoa elimu mbalimbali. Hayo yalisemwa na Afisa Utumishi, Patrick Bashemela alipokuwa akitoa utambulisho wa huduma zinazopatikana katika banda la halmashauri. “Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanatupa fursa nzuri ya kuonesha namna huduma zetu zinawafikia wananchi, banda letu linatoa huduma ya ukataji wa leseni ya biashara, elimu ya matumizi ya mfumo wa Tausi, elimu ya juu ya mikopo ya asilimia 10 na huduma ya uuzaji viwanja. Huduma zote muhimu zinazotolewa halmashauri, zitapatikana hapa kwa siku zote za maadhimisho” alisema Bashemela. Alimalizia kwa kuwakaribisha watumishi wote na wananchi kutembelea banda la halmashauri ili kupata elimu ya huduma mba...

Mexime awaonya mastaa Dodoma Jiji FC, aitaja nafasi ya tano

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA. Kocha Mkuu wa Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, Mecky Mexime amewataka wachezaji wa timu hiyo kuzingatia yale waliyojifunza kwenye uwanja wa mazoezi ili kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Singida Black Stars na waweze kutimiza malengo waliyojiwekea kwa msimu huu. Mexime aliyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo ambapo walima zabibu wa Dodoma Jiji FC watavaana na kikosi cha Singida Black Stars ikiwa ni duru ya lala salama ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, mchezo unaotarajiwa kuvurumishwa majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. “Tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huu ili tuweze kusogea nafasi za juu zaidi kwasababu nafasi ya tano bado iko wazi kwa yeyote atakayechanga karata zake vizuri ataweza kuishika. Sisi Dodoma Jiji FC mipango yetu ni kufika nafasi ya tano, kikubwa ni wachezaji kuzingatia kile tulichojifunza kwenye uwanja wa mazoezi na kuja kukionesha uwanjani” alisema Mexi...