Timu ya SHIMISEMITA ya Jiji la Dodoma yajipanga kutetea ubingwa
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Kikosi cha Timu ya Watumishi wa Jiji la Dodoma cha Mpira wa Miguu kinaendelea kujifua kwa mazoezi makali kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA 2026 yatakayofanyika jijini Mbeya, kikiwa na malengo ya kufanya vizuri na kutwaa ubingwa. Hayo aliyasema Kocha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi Jiji la Dodoma, Given Aristides wakati wa bonanza la kimichezo lililozikutanisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma, ambapo timu hizo zilipata nafasi ya kupima uwezo wao kabla ya kuingia kambini kwa ajili ya mashindano hayo. Alisema kuwa ushindani katika SHIMISEMITA unazidi kuongezeka kila mwaka kutokana na halmashauri nyingi kujiandaa kwa umakini, jambo linalowalazimu kuongeza kiwango cha mazoezi na nidhamu ili kufikia malengo waliyojiwekea. “Tunafahamu kuwa SHIMISEMITA ni mashindano yenye ushindani mkubwa, hivyo tunaendelea kujinoa kwa bidii kila siku. Bonanza hil...