Fursa uwekezaji kilimo cha Zabibu Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni kivutio kikubwa katika kilimo cha zabibu nchini kutokana na zao hilo la kibiashara kustawi vizuri na kuwanufaisha wananchi. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo mjini Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Yustina Munishi alipokuwa alielezea fursa za kilimo zinazopatikana Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Mkutano wa Baraza la Biashara Wilaya ya Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali Mtumba. Munishi aliwashauri wawekezaji na wakulima kuwekeza katika kilimo. “Zipo fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo mengi ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Tuna fursa kubwa ya uwekezaji kwenye kilimo cha zao la Zabibu. Zao la Zabibu inalimwa hapa Dodoma kwahiyo, mtu yeyote anaweza akatumia fursa hiyo kwa kuangalia maeneo yale yenye uwezekano mkubwa wa kulima zao hilo, ambayo yapo maeneo ya Hombolo Bwawani, Makulu, Chihanga, Matumbulu, Mpunguzi na Mbabala. Kwahiyo, tunaangalia ule ...