AWAMU II YA KLINIKI YA ARDHI JIJI LA DODOMA KUTATUA MIGOGORO KATA KWA KATA
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendesha Kliniki ya Ardhi kwa lengo la kutatua migogoro ya Ardhi na kuwaondolea kero wananchi. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akitoa taarifa ya katibu katika Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za utendaji kazi kwa kamati za kudumu za halmashauri kwa kipindi ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kayombo alisema “baada ya Kliniki ya Ardhi ya kwanza kufanikiwa vizuri, tumeendelea na kliniki ya pili iliyoanza Jumamosi tarehe 4 Novemba na itaendelea hadi tarehe 20 Novemba, 2023. Tumepanga watu kikata, kwa siku tunasikiliza na kuhudumia kata nne. Baada ya tarehe 20 tutajipima tena kuona tumefanikiwa kiasi gani na kama watu bado wanashida zoezi litakuwa endelevu. Tunaishukuru Wizara ya Ardhi, Nyumba na...