Posts

Showing posts from October 14, 2024

Chama cha Siasa kinawakilishwa na Wakala kituoni

Image
 

Uhamasishaji Jiji la Dodoma ni Kona kwa Kona

Image
 

Mabango ya Elimu kwa Wananchi juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yatapakaa Jiji la Dodoma

Image
 

Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma akikabidhi Mwongozo wa Uchaguzi kwa Mwakilishi wa Waandishi wa habari

Image
 

Hakuna Mamluki yeyote atakayeandikishwa kwenye orodha ya wapiga kura Jiji la Dodoma

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapiga kura. Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akifafanua mwenendo wa zoezi la uandikishaji orodha ya wapiga kura Jiji la Dodoma Kanusho hilo alilitoa ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia tuhuma zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuhusu mwenendo wa uandikishaji orodha ya wapiga kura unaoendelea wakidai kuwa kituo kimoja kiliandikisha watu kinyume na utaratibu. Dkt. Sagamiko alisema “kutokana na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, zinazoelezea kuhusu muenendo wa uandikishaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa bahati mbaya sana taarifa ile inaelezea kuhusu mwenendo mbaya wa uandikishaji. Baada ya kupitia na kusikiliza kwa makini video il...

Gari la Darasa Tembezi latembelea Dodoma Media College

Na. Asteria Frank, DODOMA Gari la Darasa Tembezi kutoka Halmashauri ya Jiji Dodoma limetembelea Dodoma Media College kwa lengo la kuelimisha kuhusu uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kuelelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Gari la Darasa Tembezi limewapa wanafunzi wa chuo hicho elimu ya kujiandikisha kwenye orodha wapiga kura zoezi liloanza tarehe 11 Oktoba, 2024 na kuendelea hadi tarehe 20 Oktoba, 2024 na kuwataka washiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwasababu ni haki yao na ni muhimu kuchagua viongozi wa mitaa wanayoishi. Mwenyekiti wa uelimishaji na uhamasishaji   wa Darasa Tembezi, Shadaiya   Hassan aliwaelimisha wanafunzi kuwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 na kusema kuwa wanatakiwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura katika ofisi za mitaa, shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya, maeneo ya wazi yenye mikusanyiko ya watu na majengo mengine ya taasisi za umma yaliyopo katika mitaa au v...

Gari la Darasa Tembezi latoa elimu Mitaa ya Jiji la Dodoma

Na. Asteria Frank, DODOMA Gari la Darasa Tembezi kutoka Halmashauri ya Jiji Dodoma linalopakia abiria kwa lengo la kuelimisha kuhusu uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kuelelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa linaendelea kuwafikia wananchi wengi katika maeneo mbalimbali ya halmashauri. Darasa Tembezi linapita kwenye kila kituo likipakia abiria na kuwapa elimu kisha linawashusha katika vituo vyao kwa kuhakikisha wameelewa zoezi la kujiandikisha katika orodha ya mpiga kura zoezi lililoanza tarehe 11-20 Oktoba, 2024 kuelekea Uchaguzi wa Serikali Mitaa. Muelimishaji na muhamasishaji wa Darasa Tembezi, Isabella Bruno aliwaeleza abira kuwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 na kusema kuwa mwananchi wanatakiwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura katika vituo vilivyopo katika ofisi za mitaa, shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya, maeneo ya wazi yenye mikusanyiko ya watu na majengo mengine ya taasisi za umma yaliyopo katik...