Mtaa wa Chikole washauriwa kujitokeza kupiga kura
Na. Faraja Mbise, MSALATO Wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wametakiwa kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi walio bora na wenye tija kwa maendeleo ya mitaa yao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Hayo, yalisemwa na mkazi wa Mtaa wa Chikole, Glory Kondo, Kata ya Msalato, alipokuwa akifanyiwa mahojiano kuhusu muitikio wa wananchi kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. “Kuna umuhimu wa kuchagua kiongozi kwasababu ni bora ukamchagua kiongozi ambae unaona kwako wewe atakufaa kuongoza vizuri, kuliko kutokupiga kura ina maana kwamba, utakuwa umeburuzwa, unaweza ukachaguliwa kiongozi ambaye ulikuwa haumuhitaji lakini itabidi ukubaliane nae kwasababu haujajiandikisha ili kuchagua kiongozi unayemtaka. Hivyo, ni muhimu kujiandikisha na ukamchagua kiongozi unayemtaka” alisema Kondo. Akiongolea kuhusu wananchi kujitokeza kupiga kura, alitoa wito kwa wakazi wote waliojiand...