SHIKUHA kutatua kero za Abiria
Na. Coletha Charles, Dodoma Katibu Mkuu wa Shirika la Kutetea Haki za Abiria nchini (SHIKUHA), Mhandisi Hashim Ramadhani, amewataka abiria kuelewa elimu na haki zao wanapotumia huduma za usafiri kwa kushirikiana na Afisa Usalama barabarani ili kuhakikisha mabasi yanazingatia sheria na huduma bora. Akizungumza katika mkutano na wajumbe wa shirika hilo kutoka mikoa mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Rafiki Hoteli jijini Dodoma, Katibu Mkuu alifafanua kampeni za elimu zimekuwa muhimu katika kuhakikisha abiria wanakuwa na uelewa wa kina kuhusu haki zao. Alisema kuwa, elimu hiyo inatolewa kupitia stendi za mabasi, masoko na sehemu zenye mikusanyiko. Pia alibainisha kuwa maafisa wa shirika hilo watashirikiana na wadau wa sekta ya usafiri kuhakikisha sheria na kanuni zinatekelezwa kwa maslahi ya abiria. āTumeweka msisitizo katika kuwaelimisha abiria juu ya jinsi ya kuripoti changamoto wanazokumbana nazo, kama vile kucheleweshwa kwa safari, kupotea kwa mizigo, au huduma zisi...