Jiji la Dodoma lavuka lengo na kukusanya 103% makusanyo ya mapato ya ndani 2023/2024
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kukusanya fedha za mapato ya ndani shilingi 51,402,342,226 sawa na asilimia 103 ya lengo la mwaka wa fedha 2023/2024 wakati ikipeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo. Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili-Juni, 2024) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kayombo ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa bajeti ya mapato ya ndani ya mwaka 2023/2024 ilikuwa shilingi 50,097,458,280. Fedha iliyokusanywa ni shilingi 51,402,342,226 sawa na asilimia 103. Alisema kati ya fedha hizo za mapato ya ndani, asilimia 73.4 ilipelekwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimi...