Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji
Na. Abdul Juma, MIYUJI Diwani wa Kata ya Miyuji, Beatrice Ngerangera amesema ujenzi wa Barabara ya kilometa sita ya kutoka Miyuji hadi Ipagala umesaidia kufikisha huduma za kijamii kwa wananchi na kuharakisha usafiri katika mazingira bora na salama. Kauli hiyo aliiotoa alipokuwa akiwaelezea waandishi wa habari mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka minne katika Kata ya Miyuji. Ngerangera alisema kuwa kilio kikubwa cha wananchi wa Miyuji ilikuwa ni barabara. “Nitumie fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utawala wake, Kata ya Miyuji imepata mambo mengi mazuri hasa ujenzi wa Barabara. Hapo zamani ilikuwa ni vigumu kupita kwenye barabara hii ila hivi sasa tunapita kwa amani. Mradi wa barabara hii yenye urefu wa kilomita sita, inaunaganisha kati ya Kata ya Miyuji na Ipagala. Hivyo, umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.7. Awali wananchi walikuwa wakipata taabu wakati wa mvua. Mimi, najisikia vizuri, kipekee...