Posts

Showing posts from April 22, 2024

Matukio Dua na Sala ya Kitaifa kuliombea Taifa la Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Dodoma

Image
 

Midahalo ya kupinga rushwa kupunguza kero kwenye jamii

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri anaendesha midahalo ya kupinga rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na kuhamasisha haki za binadamu na utawala bora ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri Hayo yalibainishwa wakati wa salamu za mkuu huyo wa wilaya kwenye hafla ya ufunguzi wa mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhusu madhara ya rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, haki za binadamu na utawala bora katika ukumbi wa St. Gaspar, Kisasa jijini Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema kuwa zipo haki za watu ambazo zinapotea kwa sababu na rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na ukatili dhidi ya watoto. “Kwa maelekezo ya mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba tushughulikie kero na tunamshukuru mkuu wa mkoa ametuongoza tumeanzisha kampeni katika mkoa wake ya ‘ kero yako, wajibu wang...

Tume ya Haki za Binadamu yasisitiza utawala bora

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA TUME ya Haki za Binadamu na Utawala bora ina dhamira kuona watanzania wanaheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na utu wa mtu. Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Dkt. Thomas Masanja Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Dkt. Thomas Masanja alipokuwa akitoa salamu za tume hiyo katika hafla ya kufungua mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhusu madhara ya rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, haki za binadamu na utawala bora katika ukumbi wa St. Gaspar Kisasa jijini Dodoma. Dkt. Masanja alisema “tunashiriki katika shughuli hii inayohusisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kwa sababu dira ya tume ni kuona jamii yenye utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na utu wa mtu. Tunataka mwisho wa siku jamii ya kitanzania inaheshimu haki za binadamu, utu wa mtu na misingi ya utawala bora”. Akiongelea ushir...

Takukuru kuwajengea moyo wa uzalendo vijana

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilianzisha klabu za kuzuia na kupambana na rushwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo kwa ajili ya kuwajengea moyo wa uzalendo na uadilifu. Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, John Joseph  Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, John Joseph alipotoa salamu wakati wa hafla ya kufungua mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhusu madhara ya rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, haki za binadamu na utawala bora katika ukumbi wa St. Gaspar Kisasa jijini Dodoma. Kamanda Joseph alisema “lengo la kuanzishwa klabu za kupinga rushwa ni kuwajengea moyo wa uzalendo vijana, kuwajenga katika uadilifu na kuongeza uelewa katika makosa na ubaya wa rushwa, kuwajengea uthubutu na ushiriki wao katika kuzuia na kupambana na rushwa. Uanzishwaji wa klabu hizo ulitokana na Takukuru kuamini kwamba vijana katika taifa ni rasilimali muhimu na chimbuko la ma...