Waziri Mavunde asisitiza miradi mikubwa ya madini iliyopewa leseni kuanza kazi haraka
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza miradi mikubwa na ya kati ya Madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa na kutimiza azma ya serikali kutoa leseni hizo. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde Aliyasema jijini Dodoma wakati akizungumza katika mkutano maalum na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya Madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla. Waziri Mavunde alisema serikali inataka kuhakikisha kuwa miradi yote ya uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa sekta binafsi kuchukua hatua kwa upande wao. āSerikali imefanya kazi yake, tumeondoa vikwazo vingi na kurahisisha utaratibu. Sasa ni juku...