Posts

Showing posts from February 25, 2024

Afisa Elimu Jiji la Dodoma anunua jina la Rais Samia kwa Laki 5

Image
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI MKUU wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Zainab Abdallah amefurahishwa na uwezo wa mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, Angel Elias alipoandika jina la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia mdomo wake na kununua jina hilo kwa shilingi 500,000. Mwanafunzi Angel Elias wa shule ya Msingi Hombolo Bwawani anayeandika kwa kutumia mdomo Furaha hiyo aliionesha katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichoambatana na utoaji tuzo za kitaaluma na kufanyika katika Shule ya Msingi St. Gasper iliyopo Miyuji jijini hapa. “Mheshimiwa Mwenyekiti kabla ya yote, ninaomba kwa ridhaa yako kama hautajari, hilo neno lililoandikwa na mtoto wangu Angel ‘I am so excited’. Nitalinunua kwa shilingi 500,000. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ni ukweli kwamba hata wale wanafunzi wasio na mahitaji maalum tunaowafundisha hawajifunzi haraka kama huyu anavyo fanya” alisisitiza Mwl. Abdallah. Akiunga mkono tukio hilo, Mkuu wa Di...

Dodoma Sec kuongeza ufaulu kula mwaka

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA SHULE ya Sekondari Dodoma imekuwa ikiongeza ufaulu kila mwaka ikifikisha zaidi ya asilimia 97 ya ufaulu wa jumla kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wanafunzi, uongozi wa shule na serikali. Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwl. Francis Tumaini alipokuwa akielezea mwenendo wa shule yake katika ufaulu Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma, Mwl. Francis Tumaini alipokuwa akielezea mwenendo wa shule yake kwa wageni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliotembelea shule hiyo kwa lengo la kujifunza. Mwl. Tumaini alisema “kwa hali ya ufaulu, tunaongeza ufaulu kila mwaka. Kwa mwaka juzi ufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu, lengo la serikali tufikie asilimia 50. Sisi tulikuwa na asilimia 65. Mwaka jana tukawa na asilimia 67 na mwaka huu tuna asilimia 68. Kwa ufaulu wa jumla kwa mwaka huu tuna asilimia zaidi ya 97. Kwa matokeo ya kidato cha Nne, tulikuwa na wanafunzi 308 tuliowasajili, ...

Tamisemi yajivumia taaluma Bunge Sekondari

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inajivunia maendeleo ya kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya wasichana Bunge kufuatia uwekezaji waliofanya na serikali shuleni hapo. Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwl. Ernest Hinju (katikati) akisisitiza jambo Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwl. Ernest Hinju alipoongoza ujumbe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kutembelea shule hiyo. Mwl. Hinju alisema “leo tulikuwa katika ziara ya kuwakaribisha na kuwatembeza wageni wetu kutoka Zanzibar ambao ni Mkurugenzi wa Elimu Maandalizi na Msingi na Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari pamoja na wasaidizi wao. Lengo ni kuja kujifunza kwa pande mbili jinsi wanavyoendesha elimu. Katika shule ya sekondari ya wasichana Bunge pamoja na mambo mengine tumeweza kuongea na wanafunzi na tumewakuta wanafunzi wanapendeza na wanahari ya kujifunza. Shule ya Sekondari ya wasichana Bunge imejen...

Msalato Sekondari wamshukuru Rais, Dkt. Samia ujenzi wa mabweni

Image
  Na. Dennis Gondwe, MSALATO SHULE ya Sekondari ya Wasichana Msalato inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu na kuwatengenezea mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia wanafunzi kwa lengo la kukuza viwango vya taaluma nchini. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Msalato, Mwl. Mwasiti Msokola alipokuwa akiongelea juhudi za serikali katika ujenzi wa miundombinu Shukrani hizo zilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Msalato, Mwl. Mwasiti Msokola alipokuwa akiongelea juhudi za serikali katika ujenzi wa miundombinu mbele ya ugeni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar uliotembelea shule hiyo. “ Tunamshukuru sana Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande wa elimu Shule ya Sekondari ya wasichana Msalato ametuona kwa sababu mwaka jana ametuletea fedha shilingi 428,000,000 kutuwezesha kujenga mabweni mawili ya maadalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano. Vilevi...

Wanafuzi Dodoma Sec watakiwa kusoma kwa bidii

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Dodoma wametakiwa kusoma kwa bidii na kutumia mfumo wa teknolojia ya ufundishaji mubashara kwa manufaa yao na vizazi vijavyo. Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Fatma Ramadhani alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Fatma Ramadhani alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma walipotembelea shule hiyo kwa ajili kujifunza juu ya mfumo wa ufundishaji mubashara unavyofanya kazi. Ramadhani alisema kuwa mfumo wa ufundishaji mubashara unawarahisishia walimu kufundisha kwa wepesi na wanafunzi kuelewa zaidi kwa sababu wanakuwa wakisikiliza na kuona. “Hivyo, ni jukumu lenu sasa wanafunzi kuweza kuhakikisha mnaitumia vizuri teknolojia hii si kwa maisha yenu pekee, bali kwa vizazi vijavyo. Kwasababu leo n...