Kata ya Chamwino kipaumbele Lishe shuleni
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO KATA ya Chamwino imetoa kupaumbele katika agenda ya lishe ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na lishe bora na kuendelea na masomo yao vizuri. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alipokuwa akiongea na walimu, wanafunzi na wadau wa masuala ya lishe katika Shule ya Msingi Chamwino iliyopo katika Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Leo ni maadhimisho ya kidunia kuhamaisha matumizi ya mimea jamii ya mikunde. Kama maharage, njegere, choroko, mbaazi. Sisi Kata ya Chamwino suala la lishe lina umuhimu mkubwa sana. Lengo ni kupinga hali ya udumavu, ukondefu na athari zote zinazotokana na lishe duni. Kata ya Chamwino tumeweka mikakati mizuri kuhakikisha wanafunzi katika shule zetu tatu za msingi na moja ya sekondari wanaweza kupata chakula shuleni. Na leo hapa tumekuja Shule ya Msingi Chamwino yenye wanafunzi takribani 2,500 kuhamasisha lishe. Na hii shule inafanya vizuri katika utoaji wa chakula shuleni, inafik...