Posts

Showing posts from February 14, 2025

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma

Na. Aisha Ibrahim, DODOMA Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Greyson Msigwa, amesema mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Dodoma, utakaoweza kubeba watu 32,000 ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 352 fedha za kitanzania, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24, chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Dodoma, uliohusisha wizara hiyo na Kampuni ya Lemonta SPA, iliofanyika kiwanja cha Changamani, Kata ya Nzuguni, jijini Dodoma. Akizungumza kuhusu lengo la ujenzi wa uwanja huo, Msigwa alisema, mradi huo ni fursa kwa maendeleo ya michezo kwa wakazi wa Jiji la Dodoma kwasababu uwanja huo utatumika katika mashindano mbalimbali kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha sekta ya michezo inazidi kukua. “Mradi huu ni fursa kwa maendeleo ya wakazi wa Dodoma lakini ni fursa kubwa kwa wanamichezo katika kukuza vipaji vyao, na sisi kama wizara tumejip...