KAMATI YA UJENZI, MANUNUZI NA MAPOKEZI JIJI LA DODOMA ZATAKIWA KUWA NA WATAALAM
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo ameagiza kamati zinazohusika na ujenzi, manunuzi na mapokezi ya vifaa kuwa na wataalam wa fani husika ili kwenda sawa na matakwa ya mwongozo wa matumizi ya āforce accountā katika kutekeleza miradi ya ujenzi. Agizo hilo alilitoa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Miyuji inayojengwa katika Kata ya Miyuji jijini Dodoma. Kayombo alisema kuwa mwongozo wa matumizi ya āforce accountā unaelekeza ziundwe kamati zenye mchanganyiko wa wajumbe na wataalam. Kamati hizo ni ujenzi, manunuzi na mapokezi ya vifaa. āKatibu wa Kamati ya Manunuzi lazima awe mtaalam wa Manunuzi. Lengo ni kuwaongoza wajumbe kwenye taratibu za Manunuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo. Kamati ya Ujenzi katibu wake anatakiwa kuwa Mhandisi na Kamati ya Mapokezi inatakiwa kuwa na mtu mwenye ujuzi wa mapokezi na utunzaji wa vifaa. Hivyo, maelekezo yangu wataalam hao waingizwe kwenye kamati ili kam...