Jiji la Dodoma kuwa kinara ushirikiano na TBS
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewataka maafisa afya na watumishi wa sekta mbalimbali kuimarisha ushirikiano na kutumia ipasavyo mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuongeza ufanisi katika ukaguzi na usajili wa bidhaa. Akifungua mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Sebastian Pima alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo washiriki kutumia mfumo wa TBS kwa usahihi ili shughuli zote za ukaguzi na usajili ziweze kufanyika kwa ufanisi kupitia mfumo huo. “Kila mmoja anatakiwa kushirikiana na wenzake, hizi ni kazi za timu, si za mtu mmoja. Tunataka Dodoma iwe mfano wa kuigwa nchini katika utekelezaji wa majukumu ya ushirikiano kati ya TBS na halmashauri, kila afisa atapangiwa malengo ya kila siku na kila wiki yatakayosaidia kuongeza utendaji na kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kuboresha huduma kwa wananchi," alisema Dkt. Pima. Aidha, aliwahimiza washiriki kutumia fursa ya uwepo wa...