Posts

Showing posts from July 30, 2023

DC SHEKIMWERI ASHAURI UTUNZAJI MAZINGIRA DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KASKAZINI -DODOMA WAKAZI wa Wilaya ya Dodoma wametakiwa kutunza na kulinda Mazingira ili kujihakikishia uhai wa maisha ya wanadamu na viumbe hai. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akipanda mti katika Zahanati ya Kikuyu Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alipoongoza zoezi la usafi wa Mazingira na upandaji miti kuzunguka Zahanati ya Kikuyu iliyopo Kata ya Kikuyu Kaskazini jijini hapa. Shekimweri alisema kuwa uhai wa wanadamu upo kwenye mazingira safi yenye miti mizuri. “Nisisitize mambo machache kwenye zoezi la kupanda miti. Katika uumbaji Mwenyezi Mungu ametuumba kwa kutegemeane na mazingira hakuna namna maisha yetu yatakuwepo pasina uwepo wa miti kwenye mazingira yanayotuzunguka. Sisi tunatoa hewa inaitwa ‘carbon dioxide’ ambayo kwa uumbaji wa Mungu hiyo ndiyo hewa safi kwa miti. Na yenyewe inatoa hewa chafu ambayo inaitwa ‘oxygen’ ambayo kwa maisha ya wanadamu ndiyo hewa safi. Kwa hiyo tunabadilishana hewa chafu ...