“Maandalizi Uandikishaji Uchaguzi Serikali za Mitaa yamekamilika” Dkt. Sagamiko
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko amesema kuwa maadalizi katika uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika kwa asilimia mia moja. Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akifafanua jambo Dkt. Sagamiko alitoa kauli hiyo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma. Msimamizi huyo alisema kuwa maandalizi katika uandikishaji kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika. Vifaa vyote vimefika na rasilimali fedha, Rais amewezesha kwa asilimia mia moja. “Kwa maandalizi, tupo timamu. Matamanio yetu tukamilishe zoezi la uandikishaji katika siku tatu” alisisitiza Dkt. Sagamiko. Aidha, aliwapongeza watumishi na wananchi waliojitokeza kwa wingi kushiriki ‘jogging’ n...