Na. Coletha Charles, KIZOTA Wananchi wa Kata ya Kizota, Halmashauri ya Jiji la Dodoma waeleza kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa makundi ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, ikiwa ni hatua ya kuinua maisha yao kiuchumi na kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Kizota, Theresia Ntui alipokuwa akiongelea mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita. Alisema kuwa tangu kuanza kwa utolewaji mikopo ya asilimia 10 katika awamu ya sita ya Rais, Dkt. Samia, Kata ya Kizota imenufaika kwa jumla ya shilingi 410,000,000 zilizotolewa kwa vikundi mbalimbali vya kijamii. Alisema kuwa katika fedha hizo, vikundi 28 vya wanawake vilipokea shilingi milioni 192, vikundi 16 vya vijana vilipewa shilingi milioni 164, na vikundi vitano vya watu wenye ulemavu vilipata shilingi milioni 49. “Mikopo hii ni yenye masharti nafuu, h...
Comments
Post a Comment