LTIP Yatambua Vipande vya Ardhi 11,000 Nzega
.jpg)
Na Magreth Lyimo, WANMM Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaotekelezwa chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi umetambua vipande vya ardhi takribani 11,000 katika Halmashauri ya Mji wa Nzega ikiwa lengo ni kutambua takribani vipande 20,000. Kiongozi wa Timu inayotekeleza M radi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Bw. Nolasko Matsuva akielezea namna mradi huo unavyotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Nzega Mkoani Tabora Hayo yalisemwa Nolasko Matsuva, Kiongozi wa Timu inayotekeleza mradi huo katika halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa Mradi huo. ‘‘Katika Halmashauri ya Mji wa Nzega utekelezaji wa Mradi ulianza na shughuli za uwandani Desemba 5, 2023 katika Mtaa wa Maporomoko, Uwanja wa ndege, Upiriri, Ushirika, mpaka sasa tuko mtaa wa Nyasa ambapo tumetambua vipande vya ardhi takribani 11,000’’ alisema Matsuva. Katika mwitikio wa wa...