Posts

Showing posts from February 25, 2025

Wananchi jijini Dodoma watarajia makubwa Kliniki ya Ardhi

Image
Na. Halima Majidi, VIWANDANI Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya Kliniki ya Ardhi ambayo inalenga kutatua changamoto za Ardhi zinazowakabili wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari katika kliniki hiyo iliofanyi viwanja vya Manispaa ya zamani, Sara Kashaji ambae ni Mkazi wa Kata ya Ipagala, alisema kuwa awali alikuwa na shamba heka mbili ukanda wa kijani, ambapo alikuwa anafanya shughuli za kilimo, shamba hilo lilichukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuahidiwa kupatiwa eneo lingine kwaajili ya kuendeleza shughuli zake za kilimo. ā€œHalmashauri walikuja kupima shamba langu, baada ya zoezi la upimaji waliahidi kutupatia maeneo wakazi wa eneo hilo, baada ya hapo tulihama na kuachia vijiji vile na kwenda sehemu nyingine, Kamishna alisema mashamba yale kuna watu wamepewa. Hivyo, sisi tusubiri kupimiwa eneo lingine Kikombo ambapo tulivyofika kule wananchi walikataa maeneo hayo, tukaambiwa tusubiri kupimiwa Makulu na mpaka sasa sijapata ufumbuziā€ alisema Kashaji. Aidha, alifafan...