Wanawake waaswa kupaza sauti unyanyasaji wa Kijinsia
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Wanawake na wasichana waaswa kutoa taarifa za unyanyasaji wa kijinsia kwa wakati pindi wanapofanyiwa ukatili huo. Hayo yalisemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Dawati la Kisheria, Rehema Mwalyambi wakati alipotembelea Kituo cha Redio A FM, wakati wa ziara ya wanawake wa Jiji la Dodoma katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni shamrashamra kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, ambapo kwa mwaka huu maadhimisho yake kitaifa yatafanyika mkoani Arusha. Mwalyambi alisema āwanawake wote pamoja na watoto wa kike tunaomba msiogope kutoa taarifa katika dawati la kijinsia lilipo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwasababu tunaona wanawake wengi wanaogopa sana kutoa taarifa pale wanapofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia. Naomba sana msiogope kwasababu sasa hivi kuna haki kwa kila mtu awe mwanamke au mwanaume, kuna sheria na adhabu pia pale tuu mtu atakapofanyiwa vitendo ukatili. Sisi kama dawati la msaada wa kisheria tupo kwaajili ya kutoa msaada kw...