Changia Damu kuokoa maisha
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wananchi wahimizwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wale wanaopata dharura ya kuhitaji huduma ya kuongezewa damu. Hamasa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Timu za Ukusanyaji Damu Kanda ya Kati, Dr. Leah Kitundya katika kliniki ya upimaji wa bure wa magonjwa yasiyoambukiza inayoendelea katika bustani ya mapumziko Nyerere Square jijini Dodoma. Alisema kuwa kila mwananchi anawajibu wa kuchangia damu kwasababu inasaidia wakati wa uhitaji. "Wananchi mliopo hapa Nyerere Square tunawaomba na kuwakumbusha kuchangia damu kwasababu itatusaidia sote wakati wa uhitaji. Damu yako inaweza kumsaidia mtu ambae hukutegemea ingemfikia. Changia kuboresha afya za wengine" alisema Dr. Kitundya. Aliwaita wananchi kuchangia damu huku akiwakumbusha kujitokeza kwa wingi kujitolea kwasababu zinapotokea ajali ama dharura za kuhitaji damu kwaajili ya kuokoa maisha wapo pia ndugu na jamaa wa karibu wanaweza kukumbwa na kadhia hiyo. "Ndugu z...