Wafanyabiashara wanufaika na ufunguzi wa Nanenane na uzinduzi wa SGR
Na. Rahma Abdallah, NANENANE NA KIKUYU KUISNI Wafanyabiashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamenufaika kutokana na ufunguzi wa maonesho ya siku ya Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma pamoja na ufunguzi wa treni ya kisasa ya mwendo kasi inayotumia umeme (SGR), ufunguzi huo uliofanyika Kata ya Kikuyu Kusini jijini Dodoma. Hayo yamezungumzwa na wafanyabiashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma mapema jana katika ufunguzi wa maonesho ya Nanenane pamoja ufunguzi wa Treni ya kisasa inayotumia umeme (SGR). “Nashukuru Mungu mimi nikiwa kama mfanyabiashara wa chakula nimenufaika sana kwa sababu watu ni mengi sana hatuna budi kumenya viazi vingi ili wateja wetu wanapokuja kukuta kila kitu kiko vizuri pia kupitia ufunguzi huu sisi kama wafanyabiashara tumepata fursa kwasababu kabla ya uzinduzi huu biashara haikuwa nzuri kabisa kwa sababu ya ukosefu wa watu (wateja) lakini kwa kupitia uzinduzi huu tumechangamkia na kufanya biashara’’ alisema ...