Posts

Showing posts from August 31, 2023

CCM CHANG’OMBE YAMPONGEZA DIWANI FUNDIKILA KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe kimempongeza Diwani wa kata hiyo Bakari Fundikila kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Chang’ombe. Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvi jijini Dodoma. Iddy alisema kuwa Kata ya Chang’ombe inapiga hatua ya maendeleo kwa kasi kutokana na Diwani wake kusimamia maendeleo. “Maendeleo haya tunayoyaona ni baada ya Diwani kusimama na kuizungumzia na kuitetea Chang’ombe. Mheshimiwa Diwani umekwenda kufanya harakati za namna gani wananchi wa Kata ya Chang’ombe wanaenda kupata huduma bora za kijamii. Leo tumekuwa na Kituo cha Afya Chang’ombe ambacho ni kituo cha mfano kwa ubora wa majengo, ukubwa wa eneo na huduma. Pale kuna jengo la mama na mtoto na huduma za upasuaji mdogo zitapelekwa” alisema Iddy. Diw...

CCM CHANG’OMBE YAPONGEZA MPANGO WA ULINZI KATIKA MITAA

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe kimepongeza mipango ya ulinzi na usalama katika mitaa ya kata hiyo na kuitaja kuwa ni mizuri. Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvu jijini Dodoma. Iddy alisema “mipango yenu kwenye ulinzi na usalama ndani ya mitaa ni mizuri. Lakini pia, mipango yenu ya kuishi na wananchi ndani ya mitaa nayo ni mizuri. Wenyeviti wa mitaa nawashukuru sana kwa hilo. Vilevile, nawashukuru watendaji wetu ngazi ya kata, Mtendaji wa Kata, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata, Afisa Ustawi wa Jamii Kata, Mratibu wa Elimu Kata, Afisa Afya Kata na wataalamu wote mnafanya kazi nzuri, kwa sababu leo Kata ya Chang’ombe ina sifa, mmeboresha mifumo ya vikundi vya ujasiriamali. Kila mtaa tumepita kuna vikundi vinavyopokea mikopo ndani ya Halmashauri yet...

CHANG’OMBE WAJIVUNIA UJENZI KITUO CHA POLISI

Image
  Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE WANANCHI wa Kata ya Chang’ombe wanajivunia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi katika kata yao jambo litakaloondoa uhalifu na kuwahakikishia usalama wao na mali zao. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy alipokuwa akiongea na wanachama wa CCM na wananchi wa Kata ya Chang’ombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvu jijini Dodoma. Iddy alisema kuwa Diwani wa Kata ya Chang’ombe, amekuwa akiipambania kata hiyo katika miradi mbalimbali ya maendeleo. “Ndugu wanachama wa CCM na wananchi, Diwani wenu Bakari Fundikila amekwenda kusimamia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe. Kituo kile takwimu zinaonesha baada ya Makao Makuu ya Polisi Wilayaya Dodoma, kinachofuata ni kituo hiki cha Polisi Chang’ombe. Na tumemsikia Diwani hapa amesema kituo hiki mmekijenga wanachama wa CCM na ...

USALAMA MTAA WA MAZENGO NI SHWARI

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE HALI ya ulinzi na usalama katika Mtaa wa Mazengo ni shwari na wananchi wanaendelea kutekeleza shughuli za maendeleo. Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mazengo, Godfrey Nkinda akisoma taarifa ya Mtaa Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mazengo, Godfrey Nkinda alipowasilosha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mazengo. Nkinda alisema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mtaa wa Mazengo uliyopo Kata ya Chang’ombe ni shwari. “Uongozi wa serikali ya Mtaa wa Mazengo umekuwa ukishirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha mtaa unakuwa salama. Polisi wamekuwa wakikabiliana na matukio madogomadogo ambayo ni viashiria vya uhalifu. Jeshi la Polisi kupitia Polisi kata na jamii wamekuwa wakifanya doria na misako ili kubaini maeneo chochezi ambayo ni vijiwe vya kuvutia bangi hasa maeneo ya Mapagale jambo ambalo Polisi wamefanikiwa kulipunguza na kazi ya kukabiliana na hali hiyo bado inaendelea” a...

DIWANI FUNDIKILA APONGEZWA UWEKEZAJI SOKO LA HAMVU

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE DIWANI wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikila amepongezwa kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika Soko la Hamvu. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chang’ombe, Bashir Iddy katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Hamvu jijini Dodoma. Iddy alisema “tunaendelea kumshukuru Diwani Bakari Fundikila kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika Soko la Hamvu, tayari ametufahamisha kuwa kiasi cha shilingi 20,000,000 zipo tayari katika akaunti ya kata kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo. Jitihada zote hizo anazifanya kwa kushirikiana na Mheshimiwa Athony Mavunde ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini. Huyu ndugu yetu Mbunge lazima tumwangalie kwa macho yote mawili kwasababu amejitoa katika kada zote ikiwemo elimu, michezo, afya na maendeleo. Sasa, maendeleo yote haya...