SERIKALI YAPONGEZWA KUTOA FEDHA UJENZI WA DODOMA ENGLISH MEDIUM
Na. Dennis Gondwe, IPAGALA KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo elimu nchini. Pongezi hizo alizitoa alipoongoza Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 kutembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Dodoma English Medium katika Kata ya Ipagala jijini Dodoma. Kaim alisema “niipongeze serikali ya awamu ya sita kwa kazi kubwa inayofanya ikiwa ni pamoja na kutenga na kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo. Tumejiridhisha na nyaraka za mradi huu baada ya kuzikagua zipo vizuri sambamba na mradi nikiri mpaka hatua hii kazi kubwa na nzuri imefanyika. Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 tumeridhia uwekaji jiwe la msingi” alisema Kaim. Akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Dodoma English medium kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awal...

Comments
Post a Comment