ELIMU JUMUISHI KUTOA FURSA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM KUSOMA JIJI LA DODOMA

Na. Dennis Gondwe, DODOMA SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kujali elimu jumuishi katika shule za awali na msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kutoa fursa kwa watoto wengi kusoma. Mwanafunzi akisaidiwa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi, Prisca Myalla (kulia) na Mkuu wa Seksheni ya Elimu Maalum, Issa Kambi (kustono) Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Awali na Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alipoongoza zoezi la kutoa kadi za bima za afya na vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Mlezi iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mwl. Myalla alisema “siku ya leo ni siku jumuishi ya kuhimiza elimu jumuishi kwenye shule zetu. Tunamshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kulisimamia hilo kwenye shule zetu kama ambavyo leo tumekusanyika hapa kugawa vifaa kwa wanafunzi wetu wenye mahitaji maalum kwa shule nane zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Tunao...