Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kupata Hati safi ya ukaguzi kwa hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2022 na kuupa heshima Mkoa wa Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akitoa maelekezo katika Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma kupitia na kujadili ripoti ya CAG Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aliposhiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kupitia na kujadili hoja za halmashauri zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Mstahiki Meya naomba nitumie nafasi hii kwa namna ya pekee na kwa idhini yako Mstahiki Meya kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kupata Hati safi ya ukaguzi kwa hesabu zinazoishia tarehe 30 Juni, 2022. Hongera sana. Hati hii safi ya ukaguzi inalifanya Jiji la Dodoma kuendelea kupata Hati safi kwa miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2017/2018. Kitendo hiki kime...