Hospitali ya Wilaya ya Dodoma kuboresha huduma za Afya
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Halmashauri ilianza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma kwa lengo la kusogeza huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Revocatus Baltazary akisoma taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Revocatus Baltazary alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma. Dkt. Baltazary alisema “kutokana na changamoto ya kukosa hospitali ya wilaya kwa muda mrefu na changamoto ya umbali wa kupata huduma za afya kwa ngazi ya wilaya, halmashauri na serikali kuu iliamua kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma ili kusogeza huduma kwa wananchi. Hatua hii itawezesha wananchi kupata huduma za afya kwa ngazi ya wilaya”. Akiongelea mapokezi ya fedha, alisema kuwa serikali kuu ilitoa kiasi cha shi...