Ukarabati tanki la Maji Kata ya Ipala waleta neema kwa wananchi
Na. John Masanja, IPALA Ukarabati mradi wa tanki la maji la Lita 90,000 katika Kata ya Ipala, waleta ahueni kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata maji kwa matumizi mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari waliofanya āmedia tourā kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Ipala kuanzia mwaka 2021 hadi 2025, Diwani George Magawa aliishukuru serikali kwa kutoa fedha shilingi 43,406,300 kwaajili ya ukarabati wa tanki la mradi mkubwa wa Maji Ipala. āWananchi sasa wanapata maji safi na salama. Kwahiyo, tunaishukuru serikali, tunamshukuru sana mbunge wetu na wataalam mbalimbali. Kata imechimba visima vinne kwaajili ya kupata maji safi na kupunguzia wananchi adha ya kutumia maji yasiyo salama. Hivi visima vinapunguza adha ya kwenda umbali mrefu kufuata maji ambayo mara nyingi siyo salama. Hivyo, wananchi wa kata yetu tatizo hili la uhaba wa maji limepungua sanaā alisema Magawa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Hombo...