Mahakama zashauriwa kuyapa uzito mashauri ya kibiashara

Na. Dennis Gondwe, DODOMA MAHAKAMA nchini zimeshauriwa kutoa umuhimu kwa mashauri ya kibiashara ili yaweze kumalizika mapema na kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kuzalisha mali. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika bustani ya Chinangali jijini Dodoma. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa Mahakama nchini ziharakishe kusilimiza mashauri ya kibiashara. “Tunapovutia mitaji na uwekezaji nchini na kufungua fursa za kibiashara, tunatambua uwekezaji kuambatana na masuala ya kisheria na migogoro ya kibiashara. Ni vema kwa Mahakama zetu kutoa umuhimu kwa mashauri ya aina hiyo pia” alisema Dkt. Hassan. ...