Vikundi vyapatiwa Mil. 215 Kata ya Mnadani

Na. Dennis Gondwe, MNADANI VIKUNDI ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu 18 vimepata mikopo ya shilingi 215,000,000 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2023 katika Kata ya Mnadani. Picha kutoka maktaba ya Jiji la Dodoma Takwimu hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Mnadani, Caroline Massawe alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mtaa wa Mnadani. Massawe alisema kuwa sekta ya maendeleo ya jamii imepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka mitatu na kuwainua wananchi wa kata hiyo. “ Kuanzia mwaka 2021 hadi sasa katika Kata ya Mnadani, vikundi 18 vimepata mikopo na shilingi 215,000,000 zimetolewa. Kati ya vikundi hivyo, vikundi sita ni vya wanawake vilivyokopeshwa shilingi 49,000,000. Vikundi tisa vya vijana vimekopeshwa shilingi 142,000,000 na vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu vimekopeshwa shilingi 24,000,000 na kufanya jumla ya shilingi 215,000,000. Mikopo hii imekuwa na manufaa...