Posts

Showing posts from September 25, 2024

Ubalozi wa Sweden kuendelea kushirikiana na Tanzania

Na. Faraja Mbise, DODOMA Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Macias ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu kutoka ofisi hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. Katika mazungumzo hayo, Balozi Macias alisema wanashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Mpango wa kunusuru Kaya Masikini nchini (TASAF), elimu na katika Taasisi za kidemokrasia. Balozi Macias aliongeza kwa kusema kuwa watashirikiana katika kutoa ujuzi na teknolojia katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aliualika Ubalozi wa Sweden kuja kuwekeza makao makuu ya nchi jijini Dodoma. Aliwaeleza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo masuala ya kilimo cha zabibu kwasababu ndio kipaumbele cha Mkoa wa Dodoma. Ziara hiyo iliambatana na zoezi la kutembelea Mji wa Serikali Mtumba, maeneo yaliyotengwa...

DC Shekimweri ahamasisha wananchi kushiriki uboreshaji daftari la wapiga kura

Na. Faraja Mbise, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Alhaj Shekimweri, aliyasema hayo katika Bonanza la wadau lililofanyika katika viwanja vya Sheli Complex iliyopo Mtaa wa Mailimbili, Kata ya Chamwino jijini Dodoma. Akizungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali Alhaj Shekimweri alisema “Kwa Jiji la Dodoma ukizingatia takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ilikuwa na wakazi karibu Laki tano kasoro, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 lilikuwa na wakazi 798,000 na ukizingatia ongezeko karibu la 3% kwa mwaka tunakaribia kufikia Milioni Moja kasoro. Takwimu zinaonesha idadi ya wapiga kura kwenye wilaya yetu ni 502,000”. Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa utoaji wa elimu kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura utakuwa ni endelev...

DC Dodoma akagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato

Na. Asteria Frank, DODOMA Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kishirikiana na Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) inatekeleza mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato. Kiwanja hiko cha Ndege cha kimataifa Cha Msalato kinajegwa kwa awamu kwa kufuata mpango mkakati wa utekelezaji wa mradi huo ukiwa na lengo la kurahisisha usafiri kati ya Tanzania na nchi jirani pamoja na uboreshaji wa usafiri wa ndani. Mkuu wa Wilaya wa Jiji la Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri alifanya ziara katika mradi huo ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wa uwanja na alisema kuwa Suma JKT wanadhamana na ujenzi huo kwaajili ya ulinzi kwa kudhibiti matendo ya wizi unaofanyika. Alisema kuwa amefarijika sana kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi na juhudi kwenye ‘package one’ ni asilimia 75 na jitihata ya ‘package’ ya pili ni asilimia 43.6. "Sehemu ya taarifa kulikiwa na changamoto na moja wapo ni udokozi wa kwenye mradi na tumepata nafasi ya kufanya mjadala mpana na kwa ...