Posts

Showing posts from February 9, 2024

PIC

 PIC

Mchengerwa: ALAT simamieni nidhamu ya Madiwani na Wakurugenzi

Image
OR-TAMISEMI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kushuka kwa nidhamu ya baadhi ya madiwani na wakurugenzi ni matokeo ya kulegalega kwa utendaji kazi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT). Waziri Mchengerwa amesema jukumu la msingi la (ALAT) ni kuimarisha nidhamu na ushirikiano baina ya baraza la madiwani na watendaji wa serikali kuhakikisha wanaongea lugha moja katika kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo. Amesema “Msingi wa uanzishwaji wa (ALAT) mwaka 1984, baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere alikusudia mengi ambayo kama (ALAT) wakifanya vizuri leo, wataweza kutusaidia kuyaboresha na kutuweka sawa”   Waziri Mchengerwa ameyasema hayo katika kikao kazi kilicho wakutanisha wajumbe wa kamati tendaji ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na viongozi wa juu wa OR – TAMISEMI na PPRA kilicholenga kujadiliana namna bora ya kuboresha utendaji kazi wa jumuiya hiyo.   Akizungumzia madai ...