Posts
Showing posts from September 24, 2026
Jukwaa la mifumo ya chakula lazinduliwa Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Rahma Magona, DODOMA Jukwaa la Mifumo ya Chakula Halmashauri ya Jiji la Dodoma limezinduliwa leo katika Hoteli ya Mesuma jijini Dodoma, likiwa na lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano wa wadau katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora na salama kwa wananchi. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, alisema kuwa jukwaa hilo litakuwa chombo cha uratibu kitakachowaunganisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kubadilishana maarifa, uzoefu na rasilimali, pamoja na kutafuta suluhisho endelevu za changamoto zinazoweza kujitokeza katika mfumo wa chakula. Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kukua kwa kasi, hali inayoambatana na ongezeko la mahitaji ya chakula bora na salama, huku mfumo wa chakula ukitegemea uzalishaji kutoka katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Mbeya, Iringa na Morogoro. Chaula alisisitiza kuwa changamoto katika mfumo wa chakula inahusisha mnyororo mzima...
Meya Chaula azindua Jukwaa la Mfumo wa Chakula Jiji la Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, amezindua rasmi Jukwaa la Wadau wa Mfumo wa Chakula katika Jiji la Dodoma kupitia Mradi wa ‘Growing Together’ unaotekelezwa na Taasisi ya Rikolto, kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali na kujadili namna ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula salama na chenye lishe katika Jiji la Dodoma. Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Mesuma, umewakutanisha wadau mbalimbali wa mfumo wa chakula, wakiwemo wakulima, wafanyabiashara, wawakilishi wa makampuni mbalimbali, taasisi na wadau wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa ajili ya kujadili kwa pamoja fursa na changamoto zinazohusu uzalishaji, upatikanaji na uhifadhi wa chakula. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meya Chaula alisema kuwa masuala ya mfumo wa chakula hayawezi kutekelezwa na mtu mmoja, bali yanahitaji ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na wadau wengine, hususan kutokana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dodo...
Wakazi Mtaa wa Mazengo wapatiwa elimu ya Lishe
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Ramadhani Mohammed, ZUZU Wakazi wa Mtaa wa Mazengo, Kata ya Zuzu jijini Dodoma, wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa watoto, ikiwa ni sehemu ya kuongeza uelewa wa jamii kuhusu ulaji wa vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya watoto. Akizungumza baada ya kupata elimu hiyo, mkazi wa Mtaa wa Mazengo, Dorice Robert Mwibala alisema kuwa elimu hiyo imewasaidia kufahamu mambo mbalimbali ambayo awali hawakuwa wakiyajua kuhusu lishe ya watoto, huku akieleza kuwa itakuwa na manufaa kwa watoto na wajukuu wao. Alisema kuwa elimu hiyo imewafurahisha kwa kuwa imewapa uelewa muhimu kuhusu namna ya kuzingatia lishe bora kwa watoto, jambo analoona linaweza kusaidia kuboresha afya na maendeleo yao. Kwa upande wake, mkazi wa Dodoma, Ibrahimu Mgeni alisema kuwa elimu hiyo atawafikishia watu wake wa karibu ili nao waweze kufahamu umuhimu wa lishe bora, huku akiomba elimu kama hiyo iendelee kutolewa mara kwa mara katika jamii. Mgeni alisema kuwa hakuna jambo bora ...
Afisa Tabibu Zahanati ya Zuzu atoa elimu ya Lishe kwa vitendo
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Ramadhani Mohammed, ZUZU Afisa Tabibu wa Zahanati ya Zuzu jijini Dodoma ametoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi kwa njia ya vitendo, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata chakula bora na chenye virutubisho muhimu kwa ukuaji na afya zao. Akitoa elimu hiyo, Afisa Tabibu huyo aliwaonesha wazazi na walezi namna ya kuchagua na kuchanganya vyakula mbalimbali vinavyopatikana katika mazingira yao ili kupata mlo kamili unaokidhi mahitaji ya mtoto. Alisema kuwa lishe bora inaanzia katika familia, hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwa na uelewa sahihi kuhusu aina ya vyakula, namna ya kuviandaa pamoja na kiasi kinachofaa kwa watoto kulingana na mahitaji yao. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia usafi wakati wa kuandaa, kupika na kuhifadhi chakula, akieleza kuwa lishe bora ikiambatana na usafi husaidia kulinda afya ya mtoto na kupunguza hatari ya magonjwa. Alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa vitendo ili kuwapa wazazi uelewa unaoweza kutumika moja kwa moja katika mais...