Wananchi Chikole wahamasishwa kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Na. Dennis Gondwe, MSALATO Wananchi wa Mtaa wa Chikole wamehamasishwa kujitokeza kushiriki zoezi la kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika maendeleo. Patrick Sebyiga (wa kwanza kushoto) akihamasisha baadhi wa wakazi wa Mtaa wa Chikole Hamasa hiyo ilitolewa na kiongozi wa timu ya hamasa ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Patrick Sebyiga alipoongoza timu hiyo kutoa hamasa kwa wananchi wa Mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato kujitokeza siku ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Sebyiga ambae pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma anaeratibu Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura. “Mtakumbuka tumemaliza zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kazi iliyobaki ni kujitokeza siku ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024. Mjitokeze kuchagua viongozi wenye sif...