Na. Dennis Gondwe, DODOMA KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imeipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa dhamira yake ya kuondoa migogoro ya Ardhi na kuwaondolea kero wananchi. Donald Mejiti (MNEC) akiongea na wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa, Kamati ya Fedha na Utawala ya Jiji la Dodoma na Menejimenti ya Jiji la Dodoma Pongezi hizo zilitolewa na kiongozi wa kamati hiyo Donald Mejiti alipoongoza Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dodoma katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mejiti alisema “tunatoa pongezi za dhati kwako Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji kwa kuonesha nia ya dhati kupunguza na kuondoa kero kwa wananchi inayotokana na migogoro ya Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Maoni yetu Chama Cha Mapinduzi ni kwamba mkishapima maeneo wekeni utaratibu mzuri wa kuyalinda ili yasivamiwe. Kuna tabia ya wananchi kuvamia maeneo yaliyopimwa na kumilikishw...