Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu yasiyokuwa na kero wala migogoro ya Ardhi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (kushoto) akikabidhi moja ya Hati zilizotolewa siku a tatu ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kuhudumiwa na kutatuliwa kero zao katika Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya tatu jijini Dodoma. Senyamule alisema “niwahakikishie Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama mwenye upendo na mama anayewapenda watanzania, jambo hili halitaki na anatamani wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu ya Dodoma na watafurahia kama watapa haki zao. Ndiyo maana amekuwa akituagiza kutatua kero zao hasa za Ardhi katika Jiji la Dodoma. Kama mkoa baada ya kupokea maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wametuagi...