Jiji la Dodoma kuanza ujenzi wa Jengo Jumuishi Kituo cha Afya Makole
Na. Faraja Mbise, MAKOLE Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatarajia kuanza ujenzi wa Jengo Jumuishi katika Kituo cha Afya Makole ambao unatarajiwa kuanza tarehe 27 Januari, 2025 chini ya Mkandarasi Mohanmmedi Builders Limited. Akizungumzia kuhusu huduma zitakazokuwa zinapatikana katika jengo hilo jumuishi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole, Dkt. Revocatus Baltazary alisema zitapatikana huduma mbalimbali kwa ajili ya kukidhi huduma zote za kiafya. “Jengo hili linaenda kujibu yote hayo, kwasababu huduma zitakazoenda kupatikana ni huduma za ‘emergency’, radiolojia, maabara, vyumba vya madaktari vitaongezwa. Pia kuna wodi za kulaza watoto chini ya umri wa miaka mitano, magonjwa ya ndani kwa wanawake na wanaume. Vilevile, wodi za upasuaji na ‘floor’ ya wakina mama wajawazito” alisema Dkt. Baltazary. Sambamba na hilo, alisema kuwa lengo hasa la kujenga jengo hilo ni kukosekana kwa baadhi ya huduma kama ‘emergency’, huduma za kulaza, na jengo la upasua. “Jengo hili linajengwa kutoka...