Posts

Showing posts from July 20, 2024

Sekondari Zuzu yapongezwa na CCM Mkoa

Image
  Na. Dennis Gondwe, ZUZU KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imewashukuru walimu wa Shule ya Sekondari Zuzu kwa kazi ya ufundishaji na kusimamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu shuleni hapo. Shukrani hizo zilitolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Donald Mejiti alipoongoza Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba nane na matundu 10 ya vyo Shule ya Sekondari Zuzu. Mejiti alisema “nianze kwa kutoa pongezi kwa kazi nzuri mliyofanya na inaonekana. Walimu wetu tunawashukuru sana kwa kazi ya kufundisha wanafunzi na kusimamia ujenzi wa miundombinu katika shule hii. Nia ya mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga majengo haya ni kuwawezesha watoto wetu wasome katika mazingira bora na salama. Watoto wetu wakisoma fursa za ajira zinakuwa nyingi. Lakini pia amejenga vyuo vya VETA ili kuongeza wigo kwa watoto wetu, bahati nzuri VETA ada yake ni nafuu sana”. Aidha, alimpongeza Mkurugenzi wa Halm...

CCM yawapongeza walimu Zuzu Sec

Image
Na. Dennis Gondwe, ZUZU KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imewashukuru walimu wa Shule ya Sekondari Zuzu kwa kazi ya ufundishaji na kusimamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu shuleni hapo. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Donald Mejiti akisisitiza jambo Shukrani hizo zilitolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Donald Mejiti alipoongoza Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba nane na matundu 10 ya vyo Shule ya Sekondari Zuzu. Mejiti alisema “nianze kwa kutoa pongezi kwa kazi nzuri mliyofanya na inaonekana. Walimu wetu tunawashukuru sana kwa kazi ya kufundisha wanafunzi na kusimamia ujenzi wa miundombinu katika shule hii. Nia ya mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga majengo haya ni kuwawezesha watoto wetu wasome katika mazingira bora na salama. Watoto wetu wakisoma fursa za ajira zinakuwa nyingi. Lakini pia amejenga vyuo vya VETA ili kuongeza wigo kwa watot...

Ukarabati Shule ya Msingi Iyumbu kupunguza msongamano darasani

Image
Na. Dennis Gondwe, IYUMBU MRADI wa ukarabati wa vyumba 10 vya madarasa katika Shule ya Msingi Iyumbu umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuwaboreshea wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Iyumbu, Mwl. Monica Nshimba Kauli hiyo ilitolewa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Iyumbu, Mwl. Monica Nshimba alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ukarabati wa vyumba 10 vya madarasa katika Shule ya Msingi Iyumbu kwa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma ilipotembelea shule hiyo iliyopo Kata ya Iyumbu jijini Dodoma. Mwl. Nshimba alisema “ukarabati wa mradi umepunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa wanafunzi darasani kwasababu kabla ya ukarabati, kulikuwa na vyumba vinne ambavyo vilikuwa havitumiki kabisa na hata vile vilivyokuwa vinatumika vilikuwa katika hali mbaya sana. Hivyo, kwa sasa vyumba vyote vinatumika. Pia mazingira ya kujifunzia na kufundishia yamekuwa mazuri na rafiki kiasi kwamba wanafunzi na walimu wote...

Kituo cha Afya Ilazo kuboresha huduma ya mama na mtoto

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI MRADI wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo utawezesha kutoa huduma za upasuaji, kliniki ya mama na mtoto na huduma za kujifungua zikiwa zimeunganishwa na mfumo wa hewa ya Oksijeni. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Revocatus Baltazary alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ilipotembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Dkt. Baltazary alisema “m radi huu utawezesha kutoa huduma za upasuaji , kliniki ya mama na mtoto, huduma za kujifungua, wodi ya watoto wachanga , huduma za kuhifadhi miili . Wodi hizi pia zimeunganishwa na mifumo ya hewa ya Oksijeni ambayo ipo katika wodi ya wazazi, watoto na jengo la upasuaji. Mifumo hii itasaidia wagonjwa wote wenye changamoto ya upumuaji kupata huduma hapa kituoni.   Aidha, huduma za lishe zitatolewa ikiwemo elimu juu ya masuala ya lishe, upimaji wa hali za lishe na ushauri”. ...

Hospitali ya Wilaya ya Dodoma kusogeza huduma kwa wananchi

Na. Dennis Gondwe, NALA Halmashauri ilianza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma kwa lengo la kusogeza huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Revocatus Baltazary alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma. Dkt. Baltazary alisema “kutokana na changamoto ya kukosa hospitali ya wilaya kwa muda mrefu na changamoto ya umbali wa kupata huduma za afya kwa ngazi ya wilaya, halmashauri na serikali kuu iliamua kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma ili kusogeza huduma kwa wananchi. Hatua hii itawezesha wananchi kupata huduma za afya kwa ngazi ya wilaya”. Akiongelea mapokezi ya fedha, alisema kuwa serikali kuu ilitoa kiasi cha shilingi 1,500,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. “Awamu ya kwanza halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 1,000,0...