Kamati za kudumu zatakiwa kuchangia kasi utekelezaji miradi ya maendeleo
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula alimtangaza Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Maadili ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa ni Omary Omary, Diwani wa Kata ya Makole, aliyepata kura zote tano kutoka kwa wajumbe wa kamati hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Omary Omary (kushoto) ambae ni Diwani wa Kata ya Makole. Kulia ni Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Bakari Fundikira ambae pia ni Diwani wa Kata ya Chang'ombe Alisema kuwa kamati hiyo ina jumla ya wajumbe watano ambao ni Omary Omary (Diwani Kata ya Makole), Swalihina Athuman (Diwani Kata ya Viwandani), Charles Ngh’ambi (Diwani Kaya ya Mbalawala), Judith Mushi (Diwani Viti Maalum) na Mwamrisho Kasule (Diwani Viti Maalum). Mstahiki Meya aliwasoma wajumbe wa kamati nyingine kuwa ni Robert Njama, Diwani wa Kata ya Mkonze na Flora Liacho, Diwani wa Viti Maalum kuwa wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Dodoma Mjini. Wengine ni Elis Kitendya, ...