Posts

Showing posts from March 14, 2025

Kata ya Makole yang’ara miaka minne ya Samia

Image
Na. Emanuel Charles, MAKOLE   Diwani wa Kata ya Makole, Omary Omary, aishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ujenzi wa barabara na ofisi ya wafanyabiashara wadogo katika kata yake.   Akizungumza katika ziara ya waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2020 hadi sasa katika Kata ya Makole, Diwani Omary alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kuijali Kata ya Makole kuwaboreshea miundombinu muhimu. “Kipekee nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miaka hii minne ambapo yupo madarakani, maboresho ambayo ametufanyia hususani sisi wana Makole kwa kutuletea miundombinu sahihi ni makubwa sana. Mheshimiwa Rais, ameboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule ya jengo la ghorofa lenye madarasa nane na ofisi mbili za waalimu katika Shule ya Msingi Makole. Katika sekta ya afya, Za...