COSTECH YAFADHILI MIRADI YA UTAFITI KUHUSU SOMO LA HISABATI

Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma. TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefadhili miradi miwili wenye thamani ya Sh.milioni 120 kwa kila mradi kwa lengo la kufanya utafiti katika somo la hisabati kutokana na matokeo mabaya ya somo hilo katika mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne. Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt.Amos Nungu Akizungumza leo Agosti 25,2023 na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema imeidhinisha miradi miwili kwa thamani ya Sh.milioni 120 kila mradi na utekelezaji wa mradi unahusisha watafiti kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini. Amefafanua mradi utafanyika katika kipindi cha miaka miwili na hatua iliyopo sasa ni kusaini mikataba. "Somo la hisabati bado ni changamoto kwani matokeo yake yamekuwa mabaya kwa kidato cha nne na darasa la saba. " Hivyo kwa kuondoa tatizo hilo Tume tumeidhinisha miradi miwili ambayo kila mmoja thamani yake ni Sh.milioni 120,"amesema na kuongeza miradi m...