Senyamule apigilia Msumari matumizi ya Nishati safi ya kupikia
Na. Mussa Richard, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ametoa wito kwa wananchi jijini Dodoma kutumia nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira na kulinda afya za wananchi kutokana na madhara ya matumizi ya nishati chafu ya kupikia. Senyamule alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Nzuguni, baada ya kufanya ziara na kukagua miradi mbalimbali ya maendelea katika kata hiyo. āRais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameshaelekeza kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia nyumbani na katika sehemu za mikusanyiko, kwahiyo kama huwezi kununua mtungi wa gesi ni bora zaidi ukatumia nishati mbadala kama makaa ya mawe na kuni poa, kwasababu upatikanaji wake na gharama zake ni nafuu na rafiki kwa kila mmoja wetu kuweza kuzimudu, hilo litasaidia kuondokana na madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya nishati chafu za kupikia, lakini pia itasaidia kutunza mazingira ya jiji letu na kuondokana na uhalibifu kama ukataji wa mkaaā alisema Seny...