Posts

Showing posts from August 15, 2023

RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATAKA KULINDA MAADILI YA JAMII

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amelitaka Kanisa la Anglikana kulinda maadili na kukemea maovu kwa vijana ili wawe raia wema katika jamii. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu jijini Dodoma  Kauli hiyo aiitoa alipokuwa mgeni rasmi katika tukio la ufunguzi wa jengo la kitega uchumi (Safina house) la Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, tukio lililofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu jijini hapa. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema “nihimize kulinda maadili na kukemea maovu katika jamii kwa vijana. Lakini wapo wakubwa wanaolitumia kanisa kufanya maovu, kemeaneni”. Aidha, Rais alilipongeza kanisa ...