Halmashauri ya Jiji la Dodoma yashiriki maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma inashiriki maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa
Umma, yanayojumuisha Taasisi za Serikali, Bunge na Mahakama, katika uwanja wa
Chinangali Park jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yanalenga kuonesha uwajibikaji wa taasisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kutoa elimu mbalimbali.
Hayo
yalisemwa na Afisa Utumishi, Patrick Bashemela alipokuwa akitoa utambulisho wa
huduma zinazopatikana katika banda la halmashauri. “Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma yanatupa fursa nzuri ya kuonesha namna huduma zetu zinawafikia
wananchi, banda letu linatoa huduma ya ukataji wa leseni ya biashara, elimu ya
matumizi ya mfumo wa Tausi, elimu ya juu ya mikopo ya asilimia 10 na huduma ya
uuzaji viwanja. Huduma zote muhimu zinazotolewa halmashauri, zitapatikana hapa
kwa siku zote za maadhimisho” alisema Bashemela.
Alimalizia
kwa kuwakaribisha watumishi wote na wananchi kutembelea banda la halmashauri
ili kupata elimu ya huduma mbalimbali na pia kupata huduma wanazohitaji.
“Napenda kuwakaribisha wote katika uwanja wa Chinangali Park hasa katika banda
la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, tunatoa huduma zote muhimu. Karibuni sana”
alimaliza Bashemela.
Maonesho
hayo yatafanyika kwa muda wa siku nane na yanatarajiwa kutoa fursa ya watumishi
kujifunza mambo mbalimbali na kupata huduma zilizosogezwa karibu kutoka katika
mabanda tofautitofauti. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo inasema “Himiza matumizi
ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji”.
MWISHO
Comments
Post a Comment